Jumapili 6 Julai 2025 - 15:54
Mashtaka dhidi ya taasisi ya utekelezaji wa sheria huko California, kwa sababu ya hatua zake dhidi ya hijabu kwa wanawake

Hawza/ Wanafunzi wawili wa Kiislamu wamewasilisha mashtaka dhidi ya taasisi ya utekelezaji wa sheria katika moja ya maeneo ya jimbo la California.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha  Shirika la Habari la Hawza, wanawake wawili Waislamu wameishtaki taasisi ya utekelezaji wa sheria katika moja ya maeneo ya California. Wameeleza kuwa walipokuwa wakishiriki katika maandamano ya amani yanayo husiana na hijabu ya wanawake, walikamatwa, na taasisi hiyo ikawalazimisha kuondoa hijabu vichwani mwao kinyume na matakwa yao.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyowasilishwa, wanafunzi hao wawili walikamatwa katika maandamano ya wanafunzi yaliyofanyika katika eneo la chuo mnamo mwezi Mei 2024.

Wachangiaji wote wawili walizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari siku ya Jumanne na kuwasilisha ushahidi wao kwa mwendesha mashtaka. Mlalamikaji wa kwanza, Salma Nasurdeen, alisema: “Niliposikia nikiamriwa nivue hijabu yangu, nilishtuka sana.” Mlalamikaji wa pili, Bi. Sheniya Aini, naye aliongeza: “Tukio hilo pia lilikuwa tukio lenye kuniumiza sana.”

Aini pia alisema: “Kwa sababu ya agizo la naibu wa taasisi hiyo, walinichukua video ili kueneza picha za nywele zangu kila mahali. Ningependa kuliweka bayana jambo hili: Hijabu yangu ni alama ya imani yangu, basi! Wanawake katika Chuo Kikuu cha Queen Mary London wanavaa hijabu. Hijabu ni andiko la wazi kabisa la Qur'an.”

Kwamba chuo kikuu kimoja huko California hakiruhusu wanawake kuvaa hijabu ni ishara ya aibu na kurudi nyuma kwa chuo hicho.

Chanzo: Yahoo News

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha